» »Unlabelled » MALENGO MAKUU YA IVST TANZANIA

 MALENGO MAKUU YA IVST



Malengo makuu ya Itifaki ya Vijana kwa Mikutano na Sherehe Tanzania (IVST) ni kama ifuatavyo:

Kukuza na kuimarisha uelewa wa itifaki, maadili na nidhamu kwa vijana katika mikutano na sherehe mbalimbali nchini Tanzania.

Kutoa mafunzo ya kitaalamu kuhusu itifaki ya mikutano, sherehe na matukio ya kijamii na kitaifa.

Kuandaa na kuendeleza vijana kuwa Maafisa wa Itifaki (Protocol Officers) wenye ujuzi na maadili.

Kukuza uongozi bora, mawasiliano yenye heshima na uwajibikaji miongoni mwa vijana.

Kushirikiana na Serikali, taasisi za umma na binafsi, pamoja na jumuiya nyingine katika masuala ya itifaki na maendeleo ya vijana.

Kukuza uzalendo, heshima ya taifa na utamaduni wa Kitanzania kupitia utekelezaji wa itifaki sahihi.

DHIMA (MOTTO / KAULIMBIU)

“Maadili, Nidhamu na Heshima katika Kila Tukio.”

Flower
KARIBU TENA

About IVST

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply