» »Unlabelled » IVST TANZANIA NININI?

 UTANGULIZI


Itifaki ya Vijana kwa Mikutano na Sherehe Tanzania (IVST) ni Jumuiya ya Kitaifa iliyo sajiliwa wizara ya Mambo ya ndani Kwa sheria ya Jumuiya za kiraia ya Mwaka 2002 na kupewa Usajili No : S.A. 24310  kwa lengo la kukuza, kusimamia na kuendeleza maadili, nidhamu na misingi ya itifaki miongoni mwa vijana nchini Tanzania. Jumuiya hii imeanzishwa kwa kutambua mchango mkubwa wa vijana katika shughuli za kijamii, kitaifa, kidini na kitaaluma, pamoja na umuhimu wa kuwa na mwongozo rasmi wa mwenendo na mpangilio katika mikutano na sherehe mbalimbali.

IVST inalenga kuwajengea vijana uwezo wa kitaaluma na kimaadili katika masuala ya itifaki, uongozi, mawasiliano na heshima ya kijamii, ili waweze kushiriki kikamilifu na kwa weledi katika maandalizi na uendeshaji wa matukio ya kitaifa na kijamii. Jumuiya hii pia inalenga kuwa chombo cha kuandaa vijana kuwa Maafisa wa Itifaki (Protocol Officers) wenye uelewa wa kina wa taratibu, heshima na hadhi ya matukio rasmi na yasiyo rasmi.

Kupitia IVST, vijana wanahamasishwa kuzingatia uzalendo, kuheshimu mila na desturi za Kitanzania, sheria za nchi, pamoja na misingi ya maadili mema, ili kujenga taswira chanya ya kizazi cha sasa na kijacho.

Flower
KARIBU TENA

About IVST

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
This is the last post.

No comments:

Leave a Reply