SEHEMU YA 1: UTANGULIZI
Itifaki ya Vijana kwa Mikutano na Sherehe Tanzania (IVST) ni Jumuiya ya Kitaifa iliyo sajiliwa wizara ya Mambo ya ndani Kwa sheria ya Jumuiya za kiraia ya Mwaka 2002 na kupewa Usajili No : S.A. 24310 kwa lengo la kukuza, kusimamia na kuendeleza maadili, nidhamu na misingi ya itifaki miongoni mwa vijana nchini Tanzania. Jumuiya hii imeanzishwa kwa kutambua mchango mkubwa wa vijana katika shughuli za kijamii, kitaifa, kidini na kitaaluma, pamoja na umuhimu wa kuwa na mwongozo rasmi wa mwenendo na mpangilio katika mikutano na sherehe mbalimbali kama:-
Kushirikiana na waandaaji wa Mikutano / Dhifa za Kitaifa na kutoa huduma ya Itifaki.
IVST inalenga kuwajengea vijana uwezo wa kitaaluma na kimaadili katika masuala ya itifaki, uongozi, mawasiliano na heshima ya kijamii, ili waweze kushiriki kikamilifu na kwa weledi katika maandalizi na uendeshaji wa matukio ya kitaifa na kijamii. Jumuiya hii pia inalenga kuwa chombo cha kuandaa vijana kuwa Maafisa wa Itifaki (Protocol Officers) wenye uelewa wa kina wa taratibu, heshima na hadhi ya matukio rasmi na yasiyo rasmi.
Kupitia IVST, vijana wanahamasishwa kuzingatia uzalendo, kuheshimu mila na desturi za Kitanzania, sheria za nchi, pamoja na misingi ya maadili mema, ili kujenga taswira chanya ya kizazi cha sasa na kijacho.
DIRA
Kuwa na Taifa endelevu lenye vijana wenye maadili na uzarendo.
DHIMA
Kuwaandaa vijana kuwa na maadili na uzalendo, kuimalisha ushirikiano baina ya ivst na mashirika ya sekta binafsi, Serikali na taasisi zake pamoja na mashirika ya Dini kwa kuzingatia mira na tamaduni za kitanzania.
MALENGO
Malengo makuu ya Itifaki ya Vijana kwa Mikutano na Sherehe Tanzania (IVST) ni kama ifuatavyo:
1. Kukuza uzalendo
2. Uongozi bora miongoni mwa vijana.
3. Mafunzo ya kitaalamu kuhusu itifaki ya mikutano, sherehe na matukio ya
kijamii na kitaifa.
4. Ushirikiano na Serikali, taasisi za umma na binafsi, pamoja na jumuiya nyingine katika masuala ya itifaki na maendeleo ya vijana.
SHUGHULI KUU
1. Kutoa mafunzo ya kitaalamu kuhusu itifaki ya mikutano, sherehe na matukio ya kijamii na kitaifa.
2. Kuwaunganisha vijana wenye taaluma ya Maafisa wa Itifaki (Protocol Officers) na fursa za kazi.
3. Kutoa elimu ya uongozi bora, mawasiliano yenye heshima na uwajibikaji miongoni mwa vijana.
4. Kutengeneza mfumo wa ushirikiano na Serikali, taasisi za umma na binafsi, pamoja na jumuiya nyinginezo katika masuala ya itifaki na maendeleo ya vijana.
5. Kutoa elimu ya maadili, utamaduni wa kitaifa na uzalendo kwa vijana.
IBARA YA 1: UANZISHWAJI WA JUMUIYA.
Inaanzishwa Jumuiya ambayo itajulikana Itifaki ya Vijana kwa Mikutano na Sherehe Tanzania (IVST) mahususi kwa lengo la Kukuza na kuimarisha uelewa wa itifaki, maadili na nidhamu kwa vijana katika mikutano na sherehe mbalimbali nchini Tanzania.


No comments: